MAOMBI

ONLINE PROPHETIC  SERVICE. 

IBADA YA KINABII MAHALI ULIPO.

KILA SIKU YA ALHAMISI MUDA KUANZA  SAA 2:00 USIKU HADI SAA 4:00 USIKU.

Kutokana Na Uhitaji Wa Watu wengi Kwenye Mtandao Wa HUDUMA YA MLANGO WA UKOMBOZI, Tumeanzisha Maombi Ya KUFUNGA Kila Siku Ya ALHAMISI Ya Kila Wiki.
Kila Mshirika Wa Huduma Hii atawajibika Kuzingatia Yafuatayo.

1.kufunga Masaa 12
2.kutuma Mahitaji Yake Siku Moja Kabla Ya Maombi Kwenye Group la Huduma.
3. Kuanza Maombi Ya Kuombea Mahitaji Kwa Watu wote MUDA Kuanzia Saa 2:00 USIKU Hadi Saa 4:00 USIKU.
4. Hakikisha Unaombea Mahitaji Ya Watu na Yako Pia Kwa Pamoja.
5. Maombi Haya Yataongozwa Na Nabii Kiongozi Wa Huduma Kwa Muda Husika
6. Hii itakua ni IBADA Kama Ibada Zingine Tunazozifanya Tofauti Yake Ni Ibada Itakayofanyika Kila Mtu Akiwa Nyumbani Kwake. Hivyo ni Ibada Itakayoambatana  Na SADAKA Siku Ya Huduma
7. Kila Wiki Kabla Ya Maombi Litatumwa Neno La Kusimamia Kwa Ajili Yako Kuomba.
8. Ibada Hii Itawahusu Watu waliokwenye MTANDAO TU wanaotoka Mbali Na Eneo Letu la Huduma.

9. Hakikisha Muda Huo Uliopangwa Unakua Nyumbani Kwako Na Umeanza Maombi.

10. Nabii Ataongoza Ibada Hii Ya KINABII Kwa Masaa Hayo

 MUHIMU.
KUHUSU DK 30 ZA KUPOKEA MUHUJIZA.

Kuanzia SAA 2:00 Hadi Saa 2:30 Hizi Zitakuwa ni DK 30 Za KUGUSA SIMU NA KUPOKEA MUHUJIZA WAKO. HIVYO Hakikisha UNAGUSA SIMU YAKO, Utaweka Simu Yako Kiganjani Kwenye SCREEN kisha Utulie Nabii Atakua Anakuombea Kwa Muda Huo.

Zingatia,.  HII Ni IBADA YA AJABU SANA KWAKO WATAKAO AMINI WATAPOKEA KWA ISHARA, AJABU NA MIHUJIZA.

KAMA UMEPOKEA UJUMBE HUU SEMA AMEN.
Kisha Tuma Mahitaji Yako KAMA Unaona Kuna MAHITAJI Ya SIRI huwezi KUTUMA Kwa GROUP Nitumie Private Kwenye Inbox.

NENO LA KUSIMAMIA WIKI HII

YEREMIA 31:21-22

BWANA ATAFANYA JAMBO JIPYA KWAKO LEO

BARIKIWA

Na Nabii.E.M Thadeo
MLANGO WA UKOMBOZI MINISTRY.
Founder.
April 2016





   IBADA YA KINABII MAHALI ULIPO.

KILA SIKU YA ALHAMISI MUDA KUANZA  SAA 2:30 USIKU HADI SAA 4:00USIKU.

Kutokana Na Uhitaji Wa Watu wengi Kwenye Mtandao Wa HUDUMA YA MLANGO WA UKOMBOZI, Tumeanzisha Maombi Ya KUFUNGA Kila Siku Ya Alhamisi Ya Kila Wiki. 
Kila Mshirika Wa Huduma Hii atawajibika Kuzingatia Yafuatayo. 

1.kufunga Masaa 12
2.kutuma Mahitaji Yake Siku Moja Kabla Ya Maombi Kwenye Group la Huduma. 
3. Kuanza Maombi Ya Kuombea Mahitaji Kwa Watu wote MUDA Kuanzia Saa 2:30 USIKU Hadi Saa 4:00 USIKU. 
4. Hakikisha Unaombea Mahitaji Ya Watu na Yako Pia Kwa Pamoja. 
5. Maombi Haya Yataongozwa Na Nabii Kiongozi Wa Huduma Kwa Muda Husika 
6. Hii itakua ni IBADA Kama Ibada Zingine Tunazozifanya Tofauti Yake Ni Ibada Itakayofanyika Kila Mtu Akiwa Nyumbani Kwake. Hivyo ni Ibada Itakayoambatana  Na SADAKA Siku Ya Huduma
7. Kila Wiki Kabla Ya Maombi Litatumwa Neno La Kusimamia Kwa Ajili Yako Kuomba. 
8. Ibada Hii Itawahusu Watu waliokwenye MTANDAO TU wanaotoka Mbali Na Eneo Letu la Huduma. 

9. Hakikisha Muda Huo Uliopangwa Unakua Nyumbani Kwako Na Umeanza Maombi. 

10. Nabii Ataongoza Ibada Hii Ya KINABII Kwa Masaa Hayo

 MUHIMU. KUHUSU DK 30 ZA KUPOKEA MUHUJIZA. 

Kuanzia SAA 2:30 Hadi Saa 3:30 Hizi Zitakuwa ni DK 30 Za KUGUSA SIMU NA KUPOKEA MUHUJIZA WAKO. HIVYO Hakikisha UNAGUSA SIMU YAKO, Utaweka Simu Yako Kiganjani Kwenye SCREEN kisha Utulie Nabii Atakua Anakuombea Kwa Muda Huo. 

Zingatia,.  HII Ni IBADA YA AJABU SANA KWAKO WATAKAO AMINI WATAPOKEA KWA ISHARA, AJABU NA MIHUJIZA. 

KAMA UMEPOKEA UJUMBE HUU SEMA AMEN.
Kisha Tuma Mahitaji Yako KAMA Unaona Kuna MAHITAJI Ya SIRI huwezi KUTUMA Kwa GROUP Nitumie Private Kwenye Inbox. 

NENO LA KUSIMAMIA WIKI HII 
LUKA 17:7-8
BWANA KUKUPATIA HAKI YAKO  UPESI

BARIKIWA

Na Nabii.E.M Thadeo 
MLANGO WA UKOMBOZI MINISTRY. 
Founder.
April 2016  



                                     MAOMBI 2016

MUONGOZO WA MAOMBI YA MFUNGO WA SIKU 30 KUOMBEA HUDUMA ZOTEZITAKAZOFANYIKA MWAKA 2016 MAOMBI HAYA YATAANZA TAREHE
10.01.2016 HADI 10.02.2016.
                                                                                                       
KICHWA CHA MAOMBI SOMO NI KUTOKA ISAYA˸ 60˸ 1-6
BWANA YESU KUTUZUKIA NA UTUKUFU WAKE KUONEKANA JUU YA HUDUMA
UTANGULIZI÷
Tunamshukuru sana Mungu kwa mara nyingine kutupatia nafasi nyeti na muhimu sana ya kuendelea na maombi haya. Huu ni mfululizo wa maombi ya kila mwaka ambayo hufanyika mwanzoni mwa mwaka. Maombi haya yametuwezesha kwa kiwango kikubwa kuinuua huduma hii  na kupitia Maombi haya tumepata mafanikio makubwa ya kihuduma.
Huu ni mwaka wanne tangu Bwana Yesu aliponipa maono haya 2011, na timu ya Huduma ya MLANO WA UKOMBOZI ikiongozwa na  Nabii E.M Thadeo inashiriki maombi haya kwa mara ya pili baada ya kuamza Huduma hii mwaka 2014.
Kwa pamoja tunashiriki katika kuhakikisha tunafunga kwa kipindi chote cha siku 30 kwa maombi ya saa 12 tukilia na Bwana juu ya huduma hii.

MWONGOZO WA MAOMBI YA TOBA (MATENDO YA MITUME 3˸ 17-21)
Neno linasema tubuni basi mrejee ili dhambi zenu zifutwezipate kuja nyakati za kuburudishwa na Bwana
Ø  Ndani ya toba kuna msamaha na Kuburudishwa hakika
Ø  Katika hatua hii lazima uzame katika toba ili Bwana aweze kuachilia na kututoa katika vifungo , uburudishwe na Bwana Yesu.
Ø  Achilia toba kwenye familia yako, ndoa,ukoo, nchi yetu
Ø  Raana za Ukoo,maagano yaliyofanyika juu yako,

2. BWANA YESU KUTUZUKIA NA UTUKUFU WAKE KUONEKANA JUU YA HUDUMA (ISAYA 60˸1 -6)
Bwana alinisemesha juu ya neno hili mwaka huu ya kuwa ni saa ya KUONDOKA na KUANGAZA kwani nuru ya Kristo inakuja.
Ni mwaka wa huduma ya MLANGO WA UKOMBOZI Kuondoka na kuangaza katika mataifa yote duniani. Katika ombi hili shughulika na mambo yafuatayo
Ø  Nuru ya Huduma ing'ae sasa katika mataifa yote.
Ø  Utukufu wa Bwana uje juu ya Huduma hii
Ø  Mataifa kujia Nuru ya MLANGO WA UKOMBOZI
Ø  Mataifa watakuja na wafalme wao kutokana na kuzuka kwa utukufu wa Bwana
Ø  Watakusanyana waje kwenye MLANGO WA UKOMBOZI -watu wengi kama bahari
Ø  Baba ainue wana kutoka mbali watakuja  LANGONI
Ø  Utajiri wa mataifa utakuja katika Huduma HII
Ø  Watu watakuja kutoka kila pande (kusi na sheba) wataleta dhahabu kwa Bwana
Ø  Sifa za Bwana zitatangazwa  kupitia hii madhabahu ya MLANGO WA UKOMBOZI
Ø  Litafanyika Lango la makimbilio kwa mataifa yote

3. MAOMBI YA KUTEKA, KUPIGA, KUTEKETEZA FALME ZA KUZIMU ZINAZOZUIA HUDUMA HII  ISAYA 8˸11-15
  1. MAOMBI YA KUFANYA MATEKA
 Mathayo 11˸12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hata sasa ufalme wa Mbinguni unatekwa na wenye nguvu. Anza kuteka ufalme wa Mungu na kuteka nguvu za giza zifanye mateka Kutoka 12˸ 36- Bwana aliwawezesha wana wa Israeli kuwateka Wamisri nyara.
·         Anza kuteka nyara falme zinazozuia Huduma
·         Teka ngome za kichawi na KIganga
·         Teka fikra za watu wanaohudhuria maombi ya Ibada za Kinabii waelewe mafundisho, watamani kukaa LANGONI Siku zote, wasiondoke kabisa, hata wakielezwa maneno ya Uzushi wasiyasadiki.
·         Fanya mateka kila roho inayoangamiza huduma.
·         Fanya mateka nguvu za kuzimu  Madhabu za Rusifer na nguvu zozote za kuzimu.
·         Fanya mateka Maeneo tunayofanyia Huduma zetu
·         Fanya mateka anga,ardhi, bahari na kuzimu
II. MAOMBI YA KUPIGA FALME  –Kutoka 12-29; Kumb 20˸ 1-4
Usiku wa manane Bwana akawapiga wazaliwa wa kwanza wa nchi yote katika Misri-kile kipigo kilisababisha Farao awape Ruhusa wana wa Israeli wakamtumikie Mungu wao.
Zipige falme zote za kipepo,kichawi,kuzimu, madhabahu za kishetani na nguvu zote ulizoziteka hapo juu.
III MAOMBI YA KUTEKETEZA NA KUANGAMIZA˸ Yer 1˸ 4-10, Kutoka 23˸ 24
Bwana anamwambia Musa yakuwa asisujudie miungu yao bali aiangamize kabisa na kuzivunja nguzo zao. Pia DANIEL 8˸ 24
·         Angamiza kila aina ya ufalme uliouteka hapo juu
·         Hakikisha unateketeza kabisa kila hila za adui juu ya huduma zisiinuke tena hizo nguvu za adui.

4. MAOMBI YA KUACHILIA ISHARA, MIUJIZA NA MAAJABU JUU YA MADHABAHU YA MLANGO WA UKOMOZI ( Yoshua 3˸ 5-7, Zab 77˸ 14, Zab 136˸4)
A. Bwana akamwambia Yoshua waambie watu wajitakase maana Bwana atatenda mambo ya ajabu kati yao. Yoshua akaliinua sanduku la agano Bwana akamtukuza mbele ya Israeli wote.
Kama vile Bwana alivyoonekana kwa Musa na Yoshua vivyo hivyo Bwana akaonekane kwetu kwa kiwango hicho hicho cha ishara na maajabukatika huduma hii.
Marko 16˸ 17 Yesu alisema na ishara hizi zitafuatana nao. Bwana aachilie ishara juu  ya Huduma
Kutoka 34˸ 10 – Bwana alisema mbele ya watu wangu wote mtatenda miujiza ya namna isiyotendeka katika dunia yote wala katika taifa lolote na watu wote unaokaa kati yao.
Matendo 19˸11- Mungu akafanya kwa mikono ya Paulo miujiza ya kupita kawaida.
Ni wakati wa MADHABAHU YA MLANGO WA UKOMBOZI kutenda miujiza mikubwa kupita kawaida
§  Magonjwa ya kila aina kuondoka juu ya watu watakaokanyaga katika madhabahu hii.
§  Pepo wachafu wa kila aina kuwatoka watu kabisa na kuachwa huru
§  Tabiri viziwi, viwete, vipofu,waliovunjika viungo,kansa,waliopooza, waliochukuliwa misukule,waliopotea na kila aina ya vifungo ni saa yao kupitia madhabahu hii kufunguliwa.
B. Maombi ya kuvunja roho za uharibifu , kuchafua, kukashifu, kupinga Madhabahu hii, zuia vifo, kafara, kudhalilishwa,kuteswa juu ya Hii Madhabahu.
katika Ombi hili hakikisha unaomba vitu vifuatavyo˸
·         Hakikisha unashughulikia kila roho ya Uhalibifu wa vyombo vya huduma na uharibifu wowote
·         Vunja roho za Kuchafua huduma kwa Maneno ya watu
·         Vunja roho za kukashifu huduma hii kwa watu
·         Roho za kupinga Madhabahu hii na kazi zote zinazofanyika hapa
·         Zuia roho za vifo kwa watu wanaokuja kuhudumiwa kwenye hii     Madhabahu hii na vifo vyovyote vya Watumishi katika Huduma hii.
·         Vunja roho za Mafarakano kwa Watumishi na Ndoa zao kisha wanaohudumiwa wasifarakane baada ya huduma
·         Kataa kila roho za udharirishaji wa aina yoyote juu ya Madhabahu n watumishi,na watu wote
·         Kataa roho za Mateso ya kila aina juu ya Madhabahu na watumishi wake.
·         Yafute maneno Yote yaliyotamkwa juu ya Hii Madhabahu.
C. Maombi ya kuachilia moto juu ya madhabahu ya mlango wa ukombozi
                                              na watumishi wake wote.                             
Walawi 6˸8-13- Bwana alisema na Musa juu ya moto wa kuteketeza sadaka kuwa moto wa madhabahuni utatunzwa uwake daima  juu ya ile madhabahu wala  wala usizimike daima
Ebrania 12˸29 Yesu kristo ni moto ulao
Achilia moto wa kristo ulao uwake katika madhabahu na watumishi wake usiku na mchana ukateketeze kila falme na nguvu za adui
Achilia nguvu ya upako kwa moto katika madhabahu.


5. MAOMBI YA KUMUOMBEA NABII E.M. THADEO-MBEBA MAONO JUU YA HUDUMA HII ANAZOZIFANYA (ISAYA 22˸20-25)
ISAYA 22˸20-25- Bwana akasema nitamwita mtumishi wangu Eliakimu namI nitamvika vasi lako (Isaya) nitamtia nguvu nitamkabidhi mamlaka yako atakuwa Baba wa wenyeji wa Yerusalemu. Omba Bwana aachilie vitu vifuatavyo kwa Nabii
Ø Amvike vazi la kinabii juu ya Huduma
Ø Amtie nguvu katika huduma zote kwa mwaka mzima
Ø Ampe mamlaka ya kuukumu Falme na Mamlka za Kuzimu.
Ø Baba ampe funguo kama alivyompa Daudi, mamlaka yawe juu ya Nabii wakati wa wote( atafunga hakuna atakayefungua)
Ø Amfanye Kiti cha utukufu katika mataifa yote
Ø  Awe imara kama msumari uliokazwa bila kutetereka katika kipindi chote cha      Huduma ( Nguzo ya chuma)
Ø Baba wa Mbinguni ampe kuketi katika Kiti cha Huduma
A.      Bwana kuachilia maono makubwa zaidi juu ya Huduma
  YOEL 2˸ 28-30 Bwana akamimine Roho wake juu ya maono Huduma tunazozifanya
B.      Ampake mafuta zaidi ya aliyompaka Daudi Mtumishi wake Zab 89˸20
C.      Ampe utiisho na Kuhofiwa kwa kiwango kikuu  Kumb 11˸20 -25

6. MAOMBI YA KUOMBEA WATUMISHI NA HUDUMA ZITAKAZOFANYIKA MWAKA JAN-DEC 2016
A). WATUMISHI, Mwambie Bwana Yesu asimamishe watumishi watakaotumika katika madhabahu hii kwa UAMINIFU Katika kipindi chote cha Huduma
Ø  Wapake mafuta ya utumishi Zab 89˸20
Ø  1Nyakati 28˸9 Watakaotumika kwa moyo wa ukamilifu
Ø  Galatia 5˸13 Watakaotumika kwa Moyo wa Upendo
Ø  1 Samwel 12˸14-15 Watakaoisikia sauti ya Kristo katika utumishi wao
Ø  Yeremia 51˸ 20-24 Bwana awafanye Rungu la Silaha za Kivita
Ø  Isaya 39˸29-31 Wenye nguvu mpya kila siku wasiochoka usiku na mchana katika Huduma
Ø  Watumishi wote watapakwa mafuta aliyopaka mafuta Nabii Kiongozi ili waweze kutumika kikamilifu katika huduma zote
Ø  Adui hatawashinda katika hududma (wasioshindwa na kitu chochote katika huduma na utumishi wao
Ø  Baba wa mbinguni awape heshima Yohana 12˸26 Mtu akimtumikia BABA wa mbinguni atakuheshimu ndoa, fedha, magonjwa n.k

7. KUOMBEA MIPANGO NA HUDUMA ZITAKAZOFANYIKA MWAKA 2016
I.MIPANGO
Ø  Kufungua TOVUTI  ya Huduma
Ø  Kununua viwanja Ekari 20 katika eneo la huduma
Ø  Kujenga Hema la maombi ukumbi wa kupokea watu 1000
Ø  Ujenzi wa shule kama kitega Uchumi cha Huduma
Ø  Kununua vyombo vya muziki vya kutosha
Ø  Kununua Viti vya kutosha watu 500
Ø  Kukamilisha usajili wa Huduma wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Ø  Kuanzisha Mradi mbalimbali ya huduma utakaowezesha huduma kukua
Ø  Kununua Gari la huduma
Ø  Ujenzi wa Miundombinu ya huduma
Ø  Kufanya huduma katika mikoa yote Tanzania bara na Visiwani na  Duniani
Ø  Kuinua waratibu wa Huduma katika mikoa yote na Duniani
Ø  Kuwahudumia wajane,Yatima na wasiojiweza kikamilifu na kuanzisha siku za wajane na Yatima kwa kukaa pamoja.
 II.HUDUMA ZOTE
Ø  Ibada za kinabii za ukombozi Jumamosi na Alhamisi- Prophetic services
Ø  Kuanzisha Ibada za uponyaji-Jumanne
Ø  Huduma zote za mikoani na safari zote
Ø  Huduma za MAJI YA UFUFUO NA UZIMA
Ø  Maombi ya kugusa TUFE LA RAMANI YA DUNIA kuita waumini kutoka Dunia kote waje kwenye Madhabahu hii.
ZINGATIA÷ Ni wakati wa  huduma kung'aa na wanaokuja watatamani kukaa hapa kumwabudu mungu marko 9˸2-7
                                                              
8. KUINUA WATU WATAKAOTEGEMEZA HUDUMA KWA FEDHA NA WAOMBAJI
(G.R.M PARTINERS)
Isaya 60˸6 ( b) Zab 72˸10, Mathayo 2˸11
Bwana alisema toka Kushi na Seba na mataifa yote watakuja wataleta  dhahabu na uvumba na kuzitangaza sifa za Bwana na kufungua hazina zao . katika hatua hii kutokana na huduma kuwa na Mahitaji mengi huku uwezo wetu kiuchumi kuwa mdogo lazima tumwombe Bwana Yesu kwa mzigo alete watu watakaomtumikia Mungu kwa fedha zao zitakazosaidia kuinua huduma.
Tamka yafuatayo÷
Ø  Waite waje kutoka pande nne za dunia
Ø Wafungulie milango ya fedha
Ø Achilia kiu yao juu ya kutoa kila walichonacho kwa Bwana juu ya madhabahu hii
Ø Vunja roho ya kukaidi maelekezo ya Roho Mtakatifu kwa kile Mungu atawasemesha watoe
Ø Omba watoe vitu kamili sio vilema au vitu visivyofaakatika madhabahu
Ø Vunja nguvu za shetani zinazowazuiya watu wasitoe vitu vyao walivyonavyo katika madhabahu hii
Ø Wapande watu hao watakaotegemeza huduma katika madhabahu
WAOMBAJI KUOMBEA MADHABAHU HII KUTOKA NJE
Ø Waite waombaji kutoka pande zote watakaotegemeza na huduma hii Kwa njia ya Maombi
Ø Achilia Roho ya kila anayekanyaga katika hii madhabahu kuombea hii madhabahu
Ø Bwana awainue waombaji wasiochoka
Ø Wasionyamaza kila siku
Ø Na kila Mwombaji atakayeiombea Madhabahu hii abarikiwe kwa kiwngo kikuu na Mungu amuinue.

9. MAOMBI YA KUOMBEA MJI WA GAIRO, TAIFA LETU NA TAIFA LA ISRAELI
Zab 122˸6, Yeremia 29˸7
Neno linasema utakieni Yerusalemu amani na wafanikiwe wakupendao. Pia utakieni amani mji ule ambao mmechukuliwa mateka, mkauombee kwa Bwana kwa maana katika  amani yake huo mji ninyi mtapata amani.
MJI WAGAIRO
Katika maombi haya lazima tuombee mji tuliopo Gairo na kisha tuuteke na kuumiliki wote sisi tukawe watawala wala hakuna mwingine. Tutazunguka Mji wote na kuutwaa kuwa mateka yetu.
Waamuzi 5˸12 Amka uwachukue mateka, ni saa ya kuchukua Gairo mateka na vitu vyake vyote ili tuumiliki.
Yoshua 8˸1-9 Bwana anautia mji wa Ai mikononi mwa mfalme. Hivyo hivyo Bwana lazima autie Gairo na viunga vyake vyote mikononi mwetu hakika.
TAIFA LA TANZANIA
Ø Amani juu ya nch yetu( Zab 122˸8)
Ø Raisi John Pombe Magufuli kutawala nchi. Pinga roho za upinzani juu yake, vifo, mikosi na balaa juu yake, mfiche kwa Damu Ya Yesu.
Ø Omba toba juu ya maasi yote yanayotendeka  umwagaji damu wa ajali zisizoisha 1 Thesalonike 5˸23
Ø Zuia roho za vita vya aina yoyote katika nchi yetu
Ø Agiza haki juu ya taifa letu Isaya 61˸11
TAIFA LA ISRAELI
Ø Kulinda Taifa la Israeli na roho za adui
Ø Watu wa Taifa hili watoke katika huzuni na machozi wanayolia
Ø Kuombea wenyeji wa Yerusalemu ambao wameishi kwa shida siku nyingi Bwana awafariji
Ø Zuia mapambano ya vikundi vya ugaidi katika Yerusalemu
Ø Bwana ashughulike na wanaoiletea hofu Israeli kutoka Mashariki ya Kati
Ø Tumuombee waziri mkuu wa Taifa la  Israeli
Ø Silaha zote zilizoinuka juu ya Israeli zisifanikiwe
Ø Futa matamko, laana, mikosi juu ya Taifa zisifanikiwe
Ø Taifa la Israeli wapokee wokovu Isaya 62˸11

10.  MAOMBI YA ULINZI NA SHURANI KWA BWANA
A. MAOMBI YA ULINZI.
Zab 66˸9, Mathayo 10˸29
Omba ulinzi toka kwa KristoYesu yeye  amesema hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote hivyo tusiogope hata kidogo nguvu za adui hazitatushinda, pia alisema hakuacha mguu wetu usogezwe hata kidogo
Ø Matendo 17˸28 Ndani ya Kristo tunaishi tunakwenda na kuwa na uhai wetu
Ø 1 Samweli 25˸29 Hata kama binadamu akiinuka bado nafsi zetu zingefungwa kwenye uhai pamoja na kristo Yesu
Ø Bwana afiche huduma zote tunazozofanya
Ø Ulinzi juu ya familia zetu
Ø Ulinzi juu ya roho ya visasi kutoka kwa adui
Ø Uhai wa watumishi ulinzi hasa katika magonjwa hakuna kuumwa kwa watumishi na familia zao zote
Ø Kila tutakapokanyaga kwenye huduma tulindwe hakika
Ø Tufichwe tusionekane sisi, watoto,ukoo, ndoa kwa damu ya Yesu
Ø Vyombo vya usafiri vyovyote tunavyitumia kila siku
Ø Vyombo vya huduma kama spika,genereta,viti na vifaa vyote vya huduma vilindwe
Ø Zuia ajali, kafara na vifo kwa watumishi katika huduma na watu tunaowahudumia hakuna vifo juu yao
Ø Ulinzi juu ya mali zote kama mashamba, ofisi na mali za ofisi
Ø Kataa kabisa Roho ya Vifo na kafara kwenye Madhabahu Hii
B. MAOMBI YA SHUKRANI
Isaya 12˸1, 1wakorinto 15˸57
Ø Tunamshukuru sana Bwana Yesu kwa kuachilia maono haya juu ya huduma kwa kipindi chote cha huduma mahali hapa tumetiwa nguvu za ushindi mkuu.
Ø Ashukuriwe atupaye kushinda 1 wako 15˸57


Maombi haya Yameandaliwa na
Nabii E.M.Thadeo.
HUDUMA YA MLANGO WA UKOMBOZI

Dec. 2015













No comments:

Post a Comment