Huduma ya Mlango wa Ukombozi ni huduma iliyoanzishwa na Nabii EM.Thadeo, Huduma ilianza mnamo mwaka 2013 baada ya Nabii kiongozi kupewa maono ya kuanzisha huduma hii. Lengo kuu la huduma hii ni watu kukombolewa katika vifungo mbalimbali vya maisha kimwili, pia Ukombozi wa Nafsi na roho ili kufikia kuurithi ufalme wa mbinguni. Makao Makuu ya Huduma yapo Gairo Morogoro Tanzania. Pia huduma hii inaongozwa na neno la Mungu kutoka katika kitabu cha Yeremia 32:6-7, "Bwana akamwambia Hanameli Jinunulie Shamba Maana Haki Ya Ukombozi ni Yako" nasi tunakiri kila atakayemwamini Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha Yake Kupitia Mlango huu wa Ukombozi ni haki yake kuwekwa Huru.
UFAFANUZI WA MLANGO WA UKOMBOZI Tafsiri ya neno Mlango (Malango) lina tafsiri nyingi hasa katika maandiko matakatifu, katika muktadha wa huduma hii tutaangalia maana ya Mlango katika maeneo makuu mawili, katika ulimwengu wa roho na ulimwengu wa Mwili.
Katika historia ya mashariki na kati utaona yakuwa miji mingi ilikua ikijengwa na kuzungushwa kuta ambapo katika kuta hizo kuliwekwa malango ambayo yalitumika kama maeneo ya kuingia na kutoka kwa ajili ya watu, wanyama na mizigo, pia yalitumika kama vizuizi vya kuzuia adui au majeshi ambapo askari walikua wakilinda masaa yote.
Ukisoma katika maandiko matakatifu utaona yakua malango ni kati ya eneo lililokuwepo katika ulimengu wa Roho, hivyo kwa mtazamo wa ulimwengu wa roho ni eneo lililopo katika ulimwengu wa Roho lililoumbwa ili litumike kwa kuingia na kutoka katika ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa kimwili ( Waebrania 11;3) ambapo yaliumbwa kwanza malango ya ulimwengu wa Roho kabla ya ulimwengu wa mwili.
KAZI ZA MLANGO/MALANGO/LANGO:
1. Malango kama eneo la kupata upenyo wa kufikia uwepo wa Mungu katika Kristo Yesu ili upate kumuabudu naye akuhudumie ( zab 100:4)
2. Mlango kama eneo la kupitisha Utukufu wa Bwana ili utukufu wa Kristo upate kuonekana mahali Mungu anataka kujulikana hivyo mara nyingi Mungu uwaongoza watu wake kuyafungua na kuyamiliki malango ya eneo Husika (zab 241)
3. Malango kama maeneo maalumu kwa ajili ya kutumiwa na Malaika katika kuwahudumia Wanadamu (Mwz 28: 12-13) Pia Ukisoma mstari wa 16 na 17 Yakobo baada ya kuota katika usingizi wake alisema kweli “ Bwana Yupo Mahali Hapa” naye akaogopa akasema Mahali hapa panatisha kama nini! Hapa ni nyumba ya mungu “ lango la Mbinguni”
Muhimu! Mara tu Yakobo alipoona na kujua hapa kuna lango na lango hilo ni la Mungu na nia yake ni kulitumia kupitisha ahadi zake kwake alihakikisha linakua wazi siku zote, hivyo Yakobo aliamua kutengeneza Madhabahu kisha kutoa sadaka ya Nadhiri juu ya ile Madhabahu iliyotengenezwa katika hilo lango.
Hivyo:- Msingi mkuu wa Huduma hii ya Mlango wa Ukombozi ni Kristo Mwenyewe kama lango la kutuhudumia na Kupitisha ahadi zake Juu ya Wanadamu! Kwa maana hivo Mtu yeyote atakayeingia na kutoka kupitia Mlango (Yesu Kristo) atawekwa huru kabisa mbali na vifungo vyote vya Maisha.
No comments:
Post a Comment